WhatsApp Messenger APK 2.25.7.3

WhatsApp Messenger

12 Feb 2025

4.5 / 204.28 Milioni+

WhatsApp LLC

Rahisi. Kibinafsi. Salama.

Pakua APK - Toleo la Hivi Karibuni

Maelezo ya kina

WhatsApp kutoka Meta ni programu ISIYOLIPISHWA ya kutuma ujumbe na kupiga simu za video. Inatumiwa na zaidi ya watu bilioni 2 katika zaidi ya nchi 180. Ni njia rahisi, ya hakika na faragha ya kutuma ujumbe, kwa hivyo unaweza kuwasiliana na ndugu na marafiki kwa wepesi. WhatsApp inafanyakazi kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta hata kama muunganisho ni wa polepole, hutakiwi kulipa ada ya kujisajili*.

Njia ya faragha ya kutuma ujumbe kote duniani

Ujumbe na simu zako za binafsi kwenda kwa ndugu na marafiki hufumbwa mwisho hadi mwisho. Hakuna mtu nje ya mawasiliano yenu, hata WhatsApp yenyewe, anaweza kuyasoma au kuyasikiliza.

Miunganisho rahisi na salama, papo hapo

Unachohitaji ni nambari yako ya simu tu, huhitaji jina la mtumiaji au vitambulishi vya kuingia. Unaweza kuona watu unaowasiliana nao ambao tayari wanaitumia WhatsApp halafu uanze kuwatumia ujumbe.

Simu za sauti na video za ubora wa juu

Piga simu salama za sauti na video zinazowajumuisha hadi watu 8 bila malipo*. Unaweza kupiga simu kati ya vifaa vya mkononi kwa kutumia Intaneti ya simu yako, hata muunganisho ukiwa wa polepole.

Soga za vikundi ili uendelee kujumuika

Endelea kujumuika na ndugu na marafiki. Soga za vikundi zilizofumbwa mwisho hadi mwisho hukuwezesha kutuma ujumbe, picha, video na hati kati ya vifaa vya mkononi na kwenye kompyuta.

Ungana mubashara

Shiriki mahali ulipo na watu ulio nao katika soga ya binafsi au ya kikundi pekee, pia unaweza kuacha kushiriki wakati wowote. Au, rekodi ujumbe wa sauti kwa mawasiliano ya haraka.

Shiriki matukio ya kila siku katika sehemu ya Hali

Hali inakuruhusu kushiriki masasisho ya maandishi, picha, video na GIF zitakazotoweka baada ya saa 24. Unaweza kuchagua kushiriki hali yako na watu wote unaowasiliana nao au wachache tu unaowachagua.

Tumia WhatsApp kwenye saa yako ya Wear OS ili kuendelea na mazungumzo, kujibu ujumbe na kupokea simu - yote kwenye mkono wako. Na, ongeza vigae na matatizo ili kufikia gumzo zako na kutuma ujumbe wa sauti kwa urahisi.


*Unaweza kulipishwa kutumia data. Wasiliana na mtoa huduma wako kwa maelezo.

---------------------------------------------------------

Ikiwa una maswali au maoni, tafadhali nenda kwenye WhatsApp > Mipangilio > Usaidizi > Wasiliana nasi

Picha za Skrini ya Programu

Matoleo ya Zamani

Sawa