Dereva wa Rida APK 12.96

Dereva wa Rida

10 Mac 2025

4.7 / 3.92 Elfu+

rida.app

Pata ajira ya udereva wa gari au boda na ujipatie pesa

Pakua APK - Toleo la Hivi Karibuni

Maelezo ya kina

Je, wewe ni dereva na unataka uwe na kipato cha ziada? Tumia programu ya Rida kupata wasafiri nchini Tanzania! Hakuna makato ya kamisheni. Mapato yote ni yako.

Fanya kazi kwa ratiba yako
Kinachofurahisha ni kwamba, bosi ni wewe! Utaamua ufanye kazi lini, hivyo, utaweza kutumia programu ya Rida kufanya kazi kila siku au kwa muda mchache nyakati za jioni.

Anza kwa haraka, mchakato ni rahisi
Ni rahisi kutumia Rida Driver. Pakua programu, jisajili na upokee maombi ya wasafiri kwa wakati halisi. Ona anapokwenda, kubali bei aliyopendekeza au kubaliana naye bei kisha endesha! Punguza muda wa kutokufanya kazi na ongeza mapato yako.

Pata bei bora zaidi
Rida inahusu tu mapatano! Wasafiri wanapopendekeza bei zao, wewe pia unaweza kupendekeza yako au ukakubali bei ya awali na ukakubali ombi la safari papo hapo.

Kwa gari na boda
Kupitia Rida unaweza kujipatia pesa kwa kuendesha gari au boda Matairi mawili au manne, yote hufanya kazi!

Pesa za haraka
Lipwa kwa pesa taslimu kwa haraka. Rida Driver huonyesha bei ya kila safari, kiasi kilichopo kwenye akaunti yako na kiasi ulichopata siku ya leo.

Picha za Skrini ya Programu

Matoleo ya Zamani

Sawa