Brave na Injini ya Utafutaji APK 1.76.73

Brave na Injini ya Utafutaji

13 Feb 2025

4.7 / 2.32 Milioni+

Brave Software

Tafuta kwenye wavuti, kwa usalama na faragha ukitumia Brave

Pakua APK - Toleo la Hivi Karibuni

Maelezo ya kina

Kikiwa kimetumiwa na watumiaji zaidi ya milioni 80, kivinjari cha Brave na injini ya utafutaji hutoa hali ya wavuti ambayo ni salama na ya faragha zaidi Ikiwa na kipengele cha kuzuia matangazo kilichojengewa ndani na VPN, Brave kwa kawaida huzuia vifuatiliaji na matangazo huku ukivinjari kwenye wavuti.

🤖 MPYA: Mratibu wa AI
Brave imezindua Brave Leo. Leo ni mratibu wa AI bila malipo ndani ya kivinjari. Uliza majibu, pata majibu, tafsiri lugha mbalimbali na zaidi.

Tafuta na Brave
Tafuta na Brave ni injini ya utafutaji ambayo ni ya faragha, huru na iliyokamilika zaidi duniani.

🙈 Kuvinjari kwa Faragha
Vinjari na usakure wavuti kwa usalama na faragha ukitumia Brave. Brave inatilia maanani sana faragha yako mtandaoni.

🚀 Vinjari Haraka
Brave ni kivinjari cha haraka! Brave hupunguza nyakati za kupakia ukurasa, huboresha utendaji wa kivinjari na kuzuia matangazo yaliyoathiriwa na programu hasidi.

🔒 Ulinzi wa Faragha
Lindwa kwa vipengele maarufu vya faragha na usalama kama vile HTTPS Everywhere (trafiki ya data iliyosimbwa kwa njia fiche), kuzuia hati, kuzuia vidakuzi na vichupo vya faragha. Udhibiti wa Faragha wa Kimataifa uliowezeshwa kwa chaguomsingi ili kuhakikisha hali zako za kisheria kutofuatiliwa mtandaoni.

🏆 Zawadi za Brave
Ukiwa na kivinjari chako cha zamani, ulilipa ili uvinjari intaneti kwa kutazama matangazo. Sasa, Brave inakukaribisha kwenye intaneti mpya. Ile ambayo wakati wako unathaminiwa, data binafsi yako inawekwa kwa faragha na unalipwa kwa sababu ya usikivu wako.

Kuhusu Brave
Dhamira yetu ni kulinda faragha yako mtandaoni kwa kuunda kivinjari salama cha haraka na faragha huku tukiongeza mapato ya matangazo kwa ajili ya watayarishaji wa maudhui. Brave inalenga kugeuza mfumo wa ikolojia wa matangazo mtandaoni kwa kutumia malipo madogo madogo na programu mpya ya kushiriki mapato ili kuwapa watumiaji na wachapishaji mkataba bora.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu Kivinjari cha Brave, tafadhali nenda kwenye www.brave.com.

Una maswali/unahitaji usaidizi?
Wasiliana nasi kupitia http://brave.com/msupport. Tunapenda kusikia maoni yako.

Sheria na Masharti: https://brave.com/terms-of-use/
Sera ya Faragha: https://brave.com/privacy/

Dokezo: Hutumia Android 7 na matoleo ya juu zaidi.

Pakua programu bora ya kivinjari cha faragha kwa ajili ya Android leo! Vinjari salama intaneti kwa ujasiri.

Picha za Skrini ya Programu

Matoleo ya Zamani

Sawa